Usajili wa Yanga 2019-2020, wachezaji wapya hawa hapa…


Ikiwa imebaki kama mwezi mmoja kwa ligi kuu Tanzania bara ianze kutimua vumbi tena hapo Agosti 23 mwaka huu , Tayari vilabu vikubwa kama Yanga na Simba vimeshakamilisha usajili wa nyota wao wapya kwa msimu mpya wa ligi kuu .

Kwa upande wa klabu ya Yanga , msimu huu inategemewa kuleta changamoto kwa wapinzani wao , hasa baada ya kufanya usajili wa nguvu. Wachezaji wapya unaotegemea kuwaona msimu ujao ni pamoja na ;-

1 . Issa Bigirimana (APR Rwanda)

Huyu ni Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga akitokea klabu ya APR ya Rwanda.

Usajili huu ulifanikishwa na mapendekezo ya Kocha Mwinyi Zahera ambaye amepewa majukumu yote hivi sasa ya kuchagua wachezaji.

2. Patrick Sibomana- (Mukura Victory Rwanda)

Huyu ni winga wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Mukura Victory Patrick ‘Papy’ Sibomana .


Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 ameichezea Mukura Victory Sports tangu Desemba mwaka jana alipoachana Shakhtyor Soligorsk ya Belarus.
Awali, Sibomana aliibukia klabu ya Isonga mwaka 2011 aliyochezea hadi mwaka 2013 alipojiunga na APR ambayo ndiyo iliyomuuza Ulaya mwaka 2017 ambako hata hivyo baada ya mwaka mmoja akarejea Rwanda.

3 . Sadney Ukhrob (Namibia)

Huyu ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Namibia

4 . Maybin Kalengo (Zambia)

Huyu ni Mshambuliaji Kinda raia wa Zambia wenye umri wa miaka 21. Kalengo amejiunga na Yanga akitokea kikosi cha ZESCO ya nchini kwao Zambia.

5 . Mustapha Suleiman- (Aigle Noir AC Haiti / Burundi)

Huyu ni beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Aigle Noir FC ya Burundi kwa mkataba wa miaka miwili

Ukiachana na hawa , wengine waliosajiliwa ni pamoja na

6 . Mohammed Camara- (Horoya Guinea)

7 . Lamine Moro (Ghana)

8 . Ally Mtoni (Lipuli FC)

9 . Kassim Khamis Abdallah (Kagera Sugar)

10. Abdulaziz Makame (Mchezaji Huru)

11 . Ally Ally (KMC)

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com