Wachezaji 10 wanaolipwa mishahara mikubwa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017


Soka ni mchezo ambao unaingiza pesa nyingi sana kwa mchezaji mwenye kipaji na kipaji chake kikapata fursa ya kuonekana . Mchezaji aliyekulia kwenye familia ya kimaskini kama Cristiano Ronaldo anayeichezea Real Madrid  anaingiza takribani bilioni 2.5 za kitanzania kwa mwezi huku ndio akiwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani .

ukiachana na mishahara ya wachezaji wa ligi kubwa duniani , vipi kuhusu hapa kwenye ligi ya Bongo ? Ukweli ni kwamba ligi ya Tanzania ndio inaongoza kwa kulipa mishahara mirefu wachezaji wake kwa upande wa Afrika Mashariki . Tusikuchoshe sana , Bongosoka.com inakuletea orodha wa wachezaji 10 wanaoingiza mishahara mirefu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017…

chirwa-wawa-mavugo-bongosoka-wachezaji-mishahara-2

10 . Vicent – Simba SC (milioni 2.1   za Kitanzania )

Vincent Atchouailou de Paul Angban , Kipa wa simba raia wa  Ivory Coast ambaye  aliwahi  kudakia timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa mika 21 kama mchezaji asiye na mkataba ambaye amepita miaka 21  anakula dola 1000 za kimarekani sawa na milioni 2.1 za kitanzania .

9 . Juuko Murshid – Simba SC (milioni 3.2   za Kitanzania )

Juuko  Murshid , Beki wa kimataifa wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda , The Cranes aliyeisaidia taifa lake la Uganda kufuzu  kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani nchini Gabon baada ya miaka 38 anakula milioni 3.2 kila mwezi akiwa na wekundu wa msimbazi .

8 . Laudit Mavugo – Simba  SC (milioni 4.3  za Kitanzania )

Baada ya Mohamed Dewji kuichangia Simba milioni 100 , klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi haikufikiria matumizi ya pesa hiyo na moja kwa moojakuamua kumshusha mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo. Mavugo anakula mshahara wa Dola za kimarekani 2000 sawa na milioni 4.3 za kitanzania .

7. John Bocco – Azam FC (milioni 5  za Kitanzania )

John Bocco ‘Adebayor’ , mchezaji aliyeipandisha Azam FC ligi kuu Tanzania bara Julai 27, 2008 anakila sababu ya kuvuta milioni 5 za kitanzania kila mwisho wa mwezi .

6. Vicent Bossou – Yanga  (milioni 7.6  za Kitanzania )

Beki wa Yanga, Vicent Bossou alijiunga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara  akitokea Goyang Hi FC ya Korea Kusini ambapo hivi sasa kila mwisho wa mwezi anakula milioni 7.6 .

5. Haruna Niyonzima – Yanga  (milioni 7.6  za Kitanzania )

Kiungo  huyu wa kimataifa wa Rwanda anaekipa katika klabu ya Dar Es Salaam Young African (Yanga) Haruna Niyonzima naye anavuta takribani milioni 7.6  kwa mwezi.

4. Amissi Tambwe – Yanga (milioni 7.6  za Tanzania)

Mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita , Amissi Tambwe alitua Yanga akitokea simba majira ya saa sita usiku wakati dirisha la usajili likielekewa kufunngwa . Tambwe , raia wa Burundi naye anaingiza milioni 7.6 za kitanzania kwa mwezi .

3. Donald Ngoma – Yanga (milioni 7.6  za Tanzania)

Aliyekua mshambuliaji tegemeo wa FC Platinum, Donald Ngoma alitua kwa vigogo wa Tanzania, Yanga SC  kwa usajili wa Dola za kimarekani 50,000. Ngoma anaingiza milioni 7.6 mwisho wa mwezi .

2. Obrey Chirwa – Yanga (milioni 10  za Tanzania)

mshambuliaji wa zamani wa  FC Platinum ,  raia wa Zambia , Obrey Chirwa alitua Yanga kwa dau la dola 100000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 za kitanzania . Chirwa anaingiza milioni 10 kila mwezi .

1 . Serge Wawa  (Milioni 15  Za Tanzania)

Beki wa kati wa Azam FC, Muivory Coast , Serge Wawa anakama mpunga mrefu kuliko mshahara anaopata rais wa sasa wa Tanzania , John  Pombe Magufuri  anayeingiza milioni 9 . 5 kwa mwezi . Wawa anakamatia dola za kimarekani elfu 7 sawa na milioni 15 za kitanzania .  Wawa ni  mmoja wa wachezaji walioipa heshima ya Ubingwa wa  CECAFA Kagame Cup  klabu yake ya Azam FC .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com