Wachezaji 16 gumzo usajili ligi kuu Tanzania Bara


LIGI inapomalizika na bingwa kupatikana, timu huanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao. Moja na maandalizi muhimu ni usajili wa wachezaji. Haya ni  majina ya wachezaji 16 wanaotajwa zaidi katika kipindi hiki cha usajili Ligi Kuu Bara.

Wachezaji-Hatari-ligi-kuu-Tanzania-bara-Bongosoka

1. Mudhamir Yassin-Mtibwa Sugar

Inadaiwa tayari ameshamwaga wino Simba. Ukimya wa viongozi wa Simba na staili yao ya usajili msimu huu ndiyo unaosababisha kutokuwa na uhakika kama kweli ameshatia mguu Msimbazi.

2. Jamal Mnyate-Mwadui FC
Pia taarifa zinasema ameshamaliza na klabu ya Simba. Winga huyu wa zamani wa Azam, Mtibwa Sugar na Mwadui, ndiye aliyefunga bao la Mwadui Simba ilipolala 1-0.

3. Hamad Juma-Coastal Union

Ni beki wa kulia aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu msimu huu akiwa na klabu ya Coastal Union, licha ya kwanza timu yake ilishuka daraja. Naye anatajwa kumalizana na Simba.

4. Elius Maguri-Stand United

Mshambuliaji wa timu ya Stand United na timu ya Taifa Taifa Stars anatajwa kuwaniwa na Majimaji ya Songea.

5. Hussein Sharrif ‘Casillas’-Mtibwa

Kipa wa zamani wa Simba anawaniwa na timu ya Prisons ya Mbeya kwenda kuziba nafasi ya Beno Kakolanya aliyechukuliwa na Yanga.

6. Atupele Green-Ndanda FC

Anatajwa kuwaniwa na timu nyingi ikiwemo Simba, Majimaji na Azam FC. Inadaiwa kuwa tayari amesajiliwa Simba.

7. Salum Telela-Yanga

Ameachwa na klabu ya Yanga, lakini ameonekana kuwa lulu kwa klabu zingine hasa Mwadui FC inayoonekana kuwa mate yanawachuruzika.

8 Miraji Adam-Coastal
Ni mchezaji wa Simba aliyekuwa anaichezea Coastal Union kwa mkopo, ingawa mkataba wake kwa sasa unaelekea ukingoni. Hata hivyo, Simba imeonyesha nia ya kutaka kumrejesha.
9. Shiza Kichuya-Mtibwa

Ni winga wa kulia wa Mtibwa Sugar anayewaniwa na Simba ingawa bado ana mkataba Mtibwa.

10. Jeremiah Juma-Prisons
Ndiye mshambuliaji bora wa Kibongo kwenye Ligi Kuu iliyomalizika. Prisons inaweza kumpoteza mchezaji huyo kwani amekuwa akiwaniwa na timu nyingi ikiwamo Simba na Azam FC

11. Hassan Kabunda-Mwadui FC
Ni winga wa kulia wa Mwadui FC. Mtoto wa beki wa zamani wa Yanga Salum Kabunda ‘Ninja’. Anatajwa kuwaniwa na klabu ya Simba.

12. Meshack Abel-KCB
Beki wa zamani wa Simba alikuwa akicheza Kenya KCB. Amerejea na anatajwa kuwaniwa na Mbeya City.

13. Idd Mobby-Mwadui FC
Anatwajwa ni mmoja wa wachezaji ambao wameshamalizana na Simba.

14. Ame Ally-Azam FC
Mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar anadaiwa kuwaniwa na klabu ya Simba.

15. Salum Kimenya-Prisons
Beki wa kulia anayeichezea Prisons, ambaye anga za michezo zinadai amemwaga wino Simba.</p>

16. Mohamed Ibrahim-Mtibwa Sugar
Kiungo kiungo mkabaji na mshambuliaji pia anadaiwa kusajiliwa na Simba.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com