Wafungaji bora ligi kuu Tanzania bara tokea mwaka 2004 na rekodi zinavyovunjwa…


Wakati msimu wa 2017/2018 ukielekea ukingoni hebu tujikumbushe rekodi za ufungaji bora ligi kuu Tanzania bara zilizowekwa tokea  mwaka 2004 .

Mshambuliaji wa Yanga , Amissi Tambwe ndio anaweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kati msimu mmoja baada ya kupachika mabao 21 katika msimu wa 2016/2017 na kuvunja rekodi iliyokaa kwa miaka 10 iliyokua ikishikiliwa na Abdallah Juma .

Juma alikuwa mshambuliaji mtaratibu, asiye na makeke uwanjani . Mpira ukitua, anaugusisha nyavu, anakimbilia kwenye kibendera.

Tambwe aliivyunja  rekodi hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City baada ya kumchungulia aliyekuwa kipa wa mbeya city kipindi hicho , Juma kaseja  nje ya 18 na kuachia shuti kali lililomshinda Kaseja .

Bao la 21 la Tambwe msimu wa 2015/2016 litakua linamuumiza kichwa Mshambuliaji hatari wa Simba ,  Emmanuel Okwi ambayo watu wengi wanadhani alishawahi kua mfungaji bora tangu atue kwenye ligi kuu Tanzania bara mwaka 2009 na kujiunga na Simba akitokea SC Villa ya Uganda na baadae kwenda nje ya nchi kisha kurejea na Yanga kisha Simba .

Ukweli ni kwamba Okwi hajawahi kuwa mfungaji bora wa msimu mwaka wowote zaidi ya kushika nafasi ya pili kwenye msimu wa 2011/2012 akiwa na mabao 12 nyuma ya John Bocco wa Azam FC (Kipindi Hicho) .

Wakati Bocco akimnyima Okwi ufungaji bora , Msimu wa 2017/2018 wachezaji hawa wako timu moja na wakibadilishana nafasi za ufungaji huku  Okwi akiwa amejipanga kuvunja rekodi ya Amissi Tambwe kwani hadi sasa hivi tayari ameshafunga mabao 19 huku zikiwa zimebakia mechi 5 kumalizila kwa msimu wa ligi kuu ambapo kuna kila dalili ya Okwi kuwa mfungaji bora wa muda wote .

List nzima ya wafungaji bora toka mwaka 2004 ni kama ifuatavyo :-

2004
Abubakar Mkangwa (Mtibwa Sugar) 16

2005
Isse Abshir (Simba) 19

2006
Abdallah Juma (Mtibwa Sugar) 20

2007-08
Michael Katende (Kagera) 11

2008-09
Boniface Ambani (Yanga) 18

2009-10
Mussa Mgosi (Simba) 18

2010/11
Mrisho Ngassa (Azam) 18

2011/12
1. Bocco (Azam) 19
2. Emmanuel Okwi (Simba) 12
3. Nsa Job (Villa) 12
4. Mutesa Mafisango (Simba) 11
5. Hamisi Kiiza (Yanga) 10

2012/13
1. Kipre Tchetche (Azam) 17
2. Dider Kavumbagu (Yanga) 10
3. Paul Nonga (Oljoro) 9
4. Jerry Tegete (Yanga) 8
5. Themi Felix (Kagera) 8

2013/14
1. Amiss Tambwe (Simba) 19
2. Kipre Tchetche (Azam) 13
3. Mrisho Ngassa (Yanga) 13
4. Elius Maguri (Ruvu) 13
5. Hamis Kiiza (Yanga) 12

2014/15
1. Simon Msuva (Yanga) 17
2. Amissi Tambwe (Yanga) 14
3. Abasrim Chidiebere (Stand) 11
4. Emmanuel Okwi (Simba) 10
5. Didier Kavumbagu (Azam) 10

2015/2016

Amissi Tambwe (Yanga) 21

2016/2017

Simon Msuva (Yanga) 14

2017/2018 (Hadi Sasa)

1. Emmanuel Okwi (Simba) 19

2. John Bocco (SImba) 14

3 . Obrey Chirwa (Yanga) 12

 

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com