Wakimataifa wawili Simba kusota Benchi kwa muda usiojulikana…


Wachezaji wawili wa kimataifa wa Simba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mussa Ndusha na Janvier Bukungu bado wataendelea kusota benchi kutokana na vibali vyao vya uhamisho wa kimataifa (ITC) kutofika hadi sasa .

Wachezaji-Simba-wakishangilia-Bao-Bongosoka

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema kuwa nyota hao hawawezi kuanza kuitumikia Simbah huku akiongeza kua kwa upande wa Simba wameshakamilisha taratibu zote zinazohitajika lakini ‘usumbufu’ umebakia kwa upande wa klabu za Kongo walizokuwa wanacheza nyota hao.

“Wakongo wamekuwa ‘wasumbufu’, mchezaji hata kama alishaondoka au alimaliza mkataba, wao wanawekwa vikwazo katika kukamilisha usajili, na hii njia ya TMS ndiyo inachelewesha zaidi,” alisema Manara.

Aliongeza kuwa Simba inaendelea kufuatilia ITC za wachezaji hao kila siku kwa sababu inahitaji kuwatumia kwenye ligi kutokana na mwalimu kuwaandaa kuwatumia katika programu zake.

Simba inaendelea kujifua kwa ajili ya kuikabili JKT Ruvu katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayofanyika Jumamosi jijini, Dar es Salaam.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com