Washindi wote 13 wa Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara na mpunga waliovuta


Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 ilifanyika jana  usiku  katika hoteli ya Double tree iliopo masaki. 

Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zimetolewa katika hafla hiyo iliofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

tuzo-ligi-kuu-bara-2015-Bongosoka

 1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu 2015/2016 ni Juma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820
 2. Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
 3. Mfungaji bora ni Amissi Tambwe wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
 4. Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein wa Simba Tsh Milioni 4.
 5. Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940
 6. Refa bora ni Ngole Mwangole Tsh Milioni 5,742,940
 7. Kocha bora ni Hans van Pluijm wa Yanga Tsh Milioni 8.
 8. Timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820
 9. Bingwa wa Ligi Kuu Yanga Tsh Milioni 81,345,723
 10. Mshindi wa pili Azam FC Tsh Milioni 40,672,861
 11. Mshindi wa tatu Simba Tsh Milioni 29,052,044
 12. Mshindi wa nne Tanzania Prisons Tsh Milioni 23, 241,635
 13. Mfungaji wa goli bora ni Ibrahim Ajib wa Simba Tsh Milioni 3

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com