Watatu wapya Simba watakaowasha moto michuano ya sportpesa..


Klabu ya wekundu wa msimbazi , Simba imeanza kwa kasi katika mbio za usajili kwa kunasa saini za wachezaji wa klabu za ndani .

Ikiwa inaelekea kucheza  na Nakuru FC hapo kesho kwenye mchezo wa kombe la Sportpesa , Simba inategemewa kuwachezesha wachezaji wake wapya waliowasajili ambao ni Jamali Mwambeleko aliyetokea Mbao Fc , Yusuph Mlipili akitokea Toto Africans na Ahmed Msumi kutoka Ndanda FC .

Simba , ambao ndio mabingwa wa kombe la shirikisho wamesisitiza kua wachezaji watakaotumika kwenye michuano ya sportpesa ni wale ambao walikua tokea mwanzo wakati kambi ya kujiandaa na michuano hiyo ilipowekwa .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com