Wenye asili ya Tanzania waliowahi kucheza kombe la dunia


Tokea Mashindano ya kombe la dunia (FIFA World Cup) yaanzishwe mwaka 1930 , Ni vijana wawili tu wenye asili ya Tanzania waliowahi kushiriki Mashindano hayo maarufu duniani ambayo ni mwaka mmoja tu umepita Tangu Ufaransa inyakue taji hilo kwa mara ya pili kwenye fainali zilizofanyika nchini Urusi .

Wafuatao ndio vijana wenye asili ya Tanzania (baba zao walikua ni watanzania ) waliowahi kushiriki mashindano hayo :-

  1. Yusuf Poulsen

Yusuph Paulsen ni moja kati ya wachezaji waliofanya vyema akiichezea timu ya taifa Denmark katika Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 .

Poulsen alifunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Peru na baadae kutawazwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Fifa.

Poulsen ndiye mchezaji wa kwanza wa asili ya Tanzania kucheza fainali za Kombe la Dunia na pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa asili ya Tanzania kufunga bao.

Poulsen kwasasa anakipiga klabu ya RB Leipzi inayoshiri ligi kuu ya ujerumani maarufu kama Bundesliga .

2 . Patrick Jan Mtiliga

Patrick Mtiliga kwasasa amestaafu soka . Alizaliwa 28 Januari 1981 ambapo babake alikuwa Mtanzania.

Mtiliga alikuwa beki na alichezea timu ya taifa ya Denmark mechi sita na alikuwa ameteuliwa kikosi cha wachezaji 23 wa kucheza Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo hakufanikiwa kucheza. Denmark waliondolewa kwenye michuano hiyo hatua ya makundi baada yao kumaliza nafasi ya tatu kundi lao.

Katika soka ya kulipwa, Alichezea klabu kadha za Denmark na Uholanzi kabla ya kuhamia Malaga ya Uhispania mwaka 2009.

Mwanzoni mwa mwaka 2010, aliumizwa kwneye pua na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid jambo lililomfanya kutocheza wiki tatu.

Aliondoka Malaga Juni 2011 baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na FC Nordsjælland ya Denmark ambapo alimalizia uchezaji wake mwaka 2015 baada ya kuwachezea mechi 150 na kufunga mabao 5.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com