Yaliyojiri ligi kuu Tanzania Bara leo..


Ligi kuu ya soka Tanzania Bara, imeendelea leo kwa mechi tano kufanyika katika viwanja mbalimbali nchini. Mechi hizi zinafanyika ili kukamilisha ratiba ya mzunguko stahiki kabla ya kuingia mapumzikoni ili kupisha mechi mbalimbali za mashindano ya kimataifa ambazo hata hivyo baadhi zimeshimamishwa kutokana na hofu ya usambaaji wa virusi vya Corona.

Singida United yazindukia Mbeya..

Baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwa upande wa Singida United, hii leo wamezinduka kutoka usingizini na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Liti (zamani Namfua), mkoani Singida.

Kabla ya mchezo wa leo, Singida United walikuwa hawajapata ushindi katika mechi nne zilizopita huku wakipoteza mechi hizo zote, ukiwemo mchezo uliopita walipofungwa 8-0 na Simba sc.

Ushindi wa leo hauwasogezi nafasi katika msimamo wa ligi kwani wanaendelea kusalia mwishoni mwa msimamo huo ( nafasi ya 20 ) na alama zao 15 pekee katika mechi 29 walizocheza.

Mabao ya Singida Utd katika mchezo wa leo, yamefungwa naye Erick Mambo 71′ na Elinywesia Sumbi 81′ huku bao pekee la Mbeya City likifungwa naye Mohamed Kapeta dakika ya 15 ya mchezo.

Mchezaji wa Biashara United na Mtibwa Sugar wakiwania mpira katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara. Picha kwa hisani ya Mtibwa Sugar na mtandao.

MATOKEO mengine leo..

IRINGA : Lipuli Fc 0-1 Kagera Sugar (Abdul Swamadi 78′) – Samora.

Moshi, KILIMANJARO : Polisi Tanzania 1-0 Ndanda Sc (Marcel Kaheza 13′ p) – Ushirika.

MOROGORO : Mtibwa Sugar 1-1 Biashara United (Jaffary Kibaya 79′ | Ramadhan Chombo 15′) – Ccm Gairo.

SHINYANGA : Mwadui Fc 2-1 Tanzania Prisons (Wallace Kiango 12′, Raphael Aloba 83′ | Samson Mbangula 90+2)

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com