Yanga kushusha Kiungo wa kimataifa leo…


SIKU chache baada ya kikosi cha Yanga kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Kagame, iliyofikia tamati jana Jumapili huku benchi la ufundi la timu hiyo likigundua kilichoimaliza, sasa limeutaka uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unamsajili kiungo mkabaji wa FC Platinum ya Zimbabwe, Thabani Kamusoko ambaye anatarajiwa kutua nchini leo Jumanne . Ipo hivi, Yanga inajua katika kikosi chake imepungukiwa kiungo mkabaji na suala hilo linafanyiwa kazi ili kupata mtu sahihi atakayemaliza tatizo hilo, lakini kwa sasa ikaona mapungufu ya kiungo wao Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na kuamua kuleta kifaa kitakachomchangamsha uwanjani. Benchi hilo la ufundi la Yanga linaloongozwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm, linadaiwa kufikia uamuzi huo hivi karibuni baada ya kukaa pamoja na uongozi na kujadili majina matatu ya viungo wakabaji waliokuwa wamependekezwa. Kiungo huyo ni Thabani Kamusoko wa FC Platinum ya Zimbabwe, ndiye aliyefunga bao pekee wakati Yanga ikiisulubu Platinum kwa mabao 5-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Thabani-Kamusoko-Yanga-FC-Platinum-zimbabwe-bongosoka

Majina mengine yaliokuwa yamependekezwa na benchi hilo la ufundi la Yanga ni pamoja na Khalid Aucho wa Gor Mahia ya Kenya pamoja na Mkenya Anthon Akumu ambaye anaitumikia Al Khartoum ya Sudan.Hata hivyo, miongoni mwa wachezaji hao, Kamusoko ndiye anadaiwa kupewa nafasi kubwa ya kujiunga na timu hiyo kutokana na kupigiwa upatu na viongozi wengi wa klabu hiyo, wakiwemo pia baadhi ya wachezeji waandamizi wa kikosi hicho cha Yanga. Kamusoko ambaye hana vitu vingi uwanjani zaidi ya ujuzi wake wa kupiga pasi za mwisho na mipira iliyokufa anakuja Yanga kufanya kazi moja ya kuwapigia pasi za mwisho mchezaji mwenzake wa zamani katika kikosi cha Platinum, Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe. Taarifa hizo zimethibitishwa na Wakala wa mchezaji huyo, Brian Moyo, aliyebahatika kuongea na gazeti la Mwanaspoti kwamba Kamusoko ni mali ya Yanga kufuatia mkataba wake na Platinum kubakiza muda mfupi kumalizika mwisho wa mwaka huu.  Moyo alisema Platinum imeridhia kumuachia Kamusoko ingawa kwa shingo upande kufuatia Wazimbabwe hao kukubaliana ni vyema kuchukua mamilioni hayo ya Yanga kuliko kumuachia kiungo huyo kuondoka bure. “Ni kweli Yanga wanahitaji huduma ya Kamusoko na tulikuwa na mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo katika wiki mbili hizi sasa na kila kitu tumekubaliana na anaweza kuja huko wiki ijayo (wiki hii),” alisema Moyo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com