YANGA kuwa fiti, inatakiwa kusajili wachezaji hawa…


Msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara ukiwa umesimama kwa siku 30 kutokana na usambaaji wa Corona, klabu mbalimbali nchini zinaendelea kupambana kuimarisha vikosi kwa msimu ujao wa ligi. Hii ni kwa kufanya makubaliano ya awali na wachezaji na timu zinazomiliki wachezaji wanaohitajika nao.

Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini, Gift Macha ameandika makala hii fupi, juu ya aina ya wachezaji ambazo Yanga wanastahili kuwasajili na namna ya kuziba mapungufu yao ya msimu huu.

Yanga imeweka rekodi moja ya ajabu msimu huu.. Imesajili wachezaji 22 katika madirisha mawili yaliyopita. Inashangaza sana. Unajua kwanini Inashangaza? Nitakwambia.

Pamoja na usajili huo mkubwa, bado hakuna cha maana ilichofanya. Mpaka sasa IPO katika nafasi ya tatu na ndoto za ubingwa zimeshayeyuka. Kwanini Yanga walifanya usajili wote huo na bado wakashindwa kufanya vizuri? Ni swali ambalo wanapaswa kujiuliza. Kuna mahali walikosea.

Kwanza, timu haiwezi kufanikiwa kwa kusajili lundo la wachezaji katika msimu mmoja.. Timu inatakiwa kujiimarisha katika maeneo kadhaa tu, dirisha baada ya dirisha.

Na ndiyo sababu nataka kuwashauri jambo Yanga.

Wakati usajili ukiwa umekaribia, ni vyema tukalisema hili mapema.. Kwa namna nilivyoitazama Yanga ya msimu huu, wala haihitaji kufanya usajili mkubwa sana mwishoni mwa msimu.

Kwanza kabisa, Yanga inatakiwa kubaki na wachezaji wote muhimu.. Isiwe kama msimu uliopita ambapo nyota walioibeba kama Ibrahim Ajib, Herritier Makambo na Gadiel Michael waliondoka. Wasiruhusu hilo msimu huu.

Pili wanahitaji kusajili mastraika wawili wa maana kuja kuziba nafasi ya Yikpe ma Molinga. Wasifanye kosa katika eneo hili.. Kama atarejea Makambo itakuwa vizuri, walete na straika mwingine wa maana tena.

Tatu, Yanga wanahitaji winga mmoja wa maana.. Winga ambaye atalingana uwezo na Bernard Morrison au angalau atamkaribia.. Asiwe winga wa kawaida kama Patrick Sibomana.

Kama watasajili Kiungo mmoja mshambuliaji itakuwa vizuri, lakini eneo muhimu zaidi ni beki mmoja wa kati na beki wa kushoto. Yule Yassin Mustapha wa Polisi Tanzania atawafaa katika upande wa kushoto.

Baada ya hapo, Yanga itakuwa imesajili wachezaji muhimu.. Hawapaswi kuzidi sita, vinginevyo itakuwa vurugu.. Wachezaji wengi waliopo Yanga wana uwezo, wanahitaji kuongezewa nguvu tu.

by @giftmacha

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com