Yanga , Simba wanawahitaji wachezaji hawa msimu ujao…


Wakati baadhi ya timu za ligi kuu zikiwa zimeanza kufanya usajili wa ligi kuu kwa msimu ujao wa 2017-2018 , Klabu kongwe za Simba na Yanga zimeonekana kua makini na wachezaji wanaowataka , huku mazungumzo mengi yakifanyika kimya kimya .

Kwa klabu ya Yanga , taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kua tayari Yanga wameanza mchakato wa kupata saini ya  baadhi ya  wachezaji wakiwemo nyota wa Simba  , IIbrahim Ajib na Jonas Mkude

Kwa upande wa Ibrahim Ajib , mkataba wake na Simba unamalizika mwezi huu, lakini pia anatakiwa na Singida United na tayari viongozi wa timu hiyo inayotarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na usajili wanaoufanya, wamekiri kufanya mazungumzo na nyota huyo.

Yanga inasaka  sahihi ya winga Haruna Chanongo wa Mtibwa Sugar, lakini pia ikidhamiria kuzibomoa Kagera Sugar na Toto Africans kuwachukua viungo Ally Nassoro na Salmin Hoza.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alikaririwa akisema kwamba usajili utafanyika kwa mapendekezo ya benchi la ufundi na kwamba lolote litakalofanyika watu wataelezwa.

Kwa upande wa wekundu wa msimbazi ,  Simba nao wapo kwenye mpango wa kusajili baadhi ya wachezaji wa Yanga , huku wakihitaji saini ya mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Haruna Niyonzima ambao wamemaliza mikataba yao.

Mbali na hao wanaotoka Yanga, mabingwa wa kombe la FA wapo kwenye hatua nzuri kuwanasa kipa Aishi Manula na beki Shomari Kapombe wa Azam. Habari za uhakika zinasema tayari John Bocco aliyemaliza mkataba Azam ameshatua Msimbazi na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Simba pia inataka kumrudisha mchezaji wake Mbaraka Yusufu aliyecheza Kagera Sugar msimu uliopita na tayari amekabidhiwa mtu maalum kushughulikia usajili huo. Aidha klabu hiyo pia inamuwania mchezaji wa Mbao FC, Mrundi Yusuf Ndikumana.

Mpaka sasa Simba ndio imeshaingia mkataba na Bocco, huku Yanga ikiendelea kufanya siri kubwa kwenye usajili wake licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda ikawaacha wachezaji zaidi ya 11, akiwepo kipa wake namba moja Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Bartez’. Inadaiwa nafasi ya Munishi Yanga itazibwa na kipa Mcameroon Youthe Rostand wa African Lyon ambayo imeshuka daraja.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com