Yanga VS Gor Mahia , ni kama fainali…


Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana katika ardhi ya Tanzania, ilikuwa ni mwaka 1996. Miaka takribani 19 imepita kabla ya kukutana tena saa chache zijazo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Yanga-Gor-Mahia-bongosoka

 

Yanga.

Hakuna shaka kila mpenzi wa Yanga, atakuwa na hamu ya kuwaona nyota kama Donald Ngoma, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, mlinzi Nadir Haroub Canavaro, Amisi Tambwe, Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke. kwa upande wa mafanikio , Yanga, imefanikiwa kutwaa taji la Kombe la Kagame mara 5, mwaka 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012. Benchi la ufundi la yanga linaongozwa na Hans Van Pluijm akisaidiwa na Charles Boniface Mkwasa.a

Gor Mahia

Gor Mahia, imeundwa na vipaji vingi kama Michael Olunga, Meddie Kagere, Mlinda mlango Boniface Oluoch na mlinzi George Odhiambo. Kwa upande wa mafanikio , Mara ya mwisho kutwaa taji hili ilikuwa ni 1985, imefanikiwa kujinyakulia taji hili mara 5, mwaka 1976, 1977, 1980, 1981 na 1985. Benchi la ufundi la Gor Mahia linaongozwa na kocha Frank Nattal.

Mchezo ndani ya dakika 90.

Nionavyo, mchezo huu utakuwa mgumu kwa timu zote mbili, mara ya mwisho kukutana katika ardhi ya Tanzania, Yanga ilikubali kibano cha goli 4-0 kutoka kwa Gor Mahia. Ikumbukwe ulikuwa ni mchezo kuwania mshindi wa tatu. Hapo awali walipangwa kundi moja na mchezo baina yao ulimalizika kwa sare ya goli 1-1. Mchezo huu utaamuliwa kwa kiasi kikubwa na nidhamu ndani ya uwanja kwa dakika zote 90, atakayeruhusu kufanya makosa ya kizembe, anaweza akaadhibiwa wakati wowote. Pia itategemea jinsi ambavyo mabenchi ya ufundi ya timu zote, zitakavyo waandaa wachezaji wao kimbinu, kiakili na kisaikolojia. Vinginevyo hii ni kama fainali, Yanga atahitaji kulipiza kisasi huku Gor Mahia wakitaka kuanza vema michuano hiyo. Mpira ni dakika 90, tusubiri tujionee.

 

->Makala hii imeandikwa na Halidi Abdulrahman.

 

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com