Yanga wanakibarua kigumu dhidi ya Mbao FC leo


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara , leo watakua na kibarua kigumu pale watakapowavaa wenyeji Mbao FC kwenye mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye dimba la CCM Kirumba , Jijini Mwanza .

Mechi ya leo itakua ngumu kwa yanga pale watakapojaribu kuukata mzizi wa kufungwa kwani katika mechi zote mbili ilizocheza na mbao FC kwenye uwanja huo , ilipoteza zote .

Naye Kocha msaidizi wa Yanga , Shadrack Nsajigwa amekaririwa akisema kuwa wataingia katika mchezo wa leo bila hofu yoyote ya kupoteza .huku akisisitiza kikosi chake kiko fiti kuondoka na pointi 3 muhimu .

Baada ya mechi za jana , Yanga inaendelea kushikilia nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 21 sawa na Mtibwa sugar inayoshika nafasi ya nne kwa tofauti ya idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga .

Kwa upande wa Mbao FC , yenyewe inashikilia nafasi ya 8 huku ikiwa tayari imeshajikusanyia pointi 11 katika michezo 11 iliyokwisha cheza .

Yanga itaingia dimabi leo bila nyota wake sita ambao ni Ibrahim Ajib , Donald Ngoma , Obrey Chirwa , Thabani Kamusoko , Beno kakolanya na Kelvin Yondani . Pia Kocha mkuu wa Yanga , George Lwandamina hatokuwepo kutokana na kusafiri kwenda Zambia kwenye msiba wa mtoto wake .

Michezo mingine ya Ligi Kuu itakayopigwa leo ni pamoja na  Njombe Mji FC itakayoikaribisha Singida United Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe kuanzia Saa 8:00 mchana, wakati Jumatatu Mbeya City watawakaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Mwadui Compex, Kishapu.

Baada ya raundi ya 12, Ligi Kuu ya Vodacom itapisha mechi za Kombe la Mapinduzi na raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia raundi ya 13 itakayofanyika kati ya Januari 13 na 17, 2018.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com