Yanga yaanza vizuri Mapinduzi Cup


Klabu ya Yanga imeanza vizuri mashindano ya kombe la mapinduzi kwa kukaa kileleni mwa kundi B baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1 – 0 . dhidi ya KVZ .

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Shaban Mohamed dakika ya 78 ya mchezo akimalizia pazi nzuri ya Matheo Simon .

Kwa ushindi huo , Yanga watakua kwenye hali nzuri pale watakapokutana na Azam FC , Keshokutwa , Januari 5 , baada ya Azam FC kutoa sare dhidi ya Jamhuri kwenye mchezo wao wa ufunguzi .

Michuano ya Kombe la Mapinduzi itaendelea leo kwa mchezo kati ya Simba SC na Chipukizi kuanzia Saa 2:15 usiku, ambao utatanguliwa ne mechi kati ya Jamhuri na Malindi Saa 10:15 jioni.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com