Yanga yaichapa Toto Africans 1- 0 , Ubingwa wa ligi kuu nje nje…


Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi  kuu Tanzania bara kwa mara ya  tatu mfululizo baada ya kuifunga klabu ya Toto Africans goli 1 – 0 katika mchezo  wa ligi kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa ushindi wa leo , Yanga wanafikisha pointi 68 huku wakiongoza ligi nyuma ya Simba SC yenye pointi 65 ambapo wote wanamichezo 29 waliyochezwa .

Hivi sasa Yanga wanaweza kuanza kushangilia ubingwa kwani kuupoteza itahitaji wafungwe na mbao FC huku Simba wakihitaji ushindi wa goli 12  – 0 kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya mwadui FC .

Kwenye mchezo wa leo , Toto Africans waliingia uwanjani wakiwania kutoshuka daraja huku Yanga wakiwania ubingwa . Hali hiyoilisababisha milango kua migumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika .

Kipindi cha pili cha Mchezo wakati kila mtu akihesabu mchezo utaisha bila kufungana , Amissi  Tambwe  aliweza kuwanyayua mashabiki wa Yanga dakika ya 81 ya mchezo baada ya  kufunga bao kwa kichwa akimalizia krosi safi iliyopigwa na kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Mechi za mwisho za ligi kuu zitapigwa zote siku ya Jumamosi , tarehe 2o , Mwezi huu ambapo ndio siku ambayo bingwa wa ligi kuu Tanzania bara atakabidhiwa kombe lake .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com