Yanga yaipa kichapo Mlandege


Klabu ya Yanga wakiwa kisiwani Zanzibar kwa kambi ya wiki moja Jana walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 4 – 1 dhidi ya Mlandege .

Mchezo huu ulikua ni wa kujiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Patrick Sibomana dakika ya 26, Juma Balinya dakika ya 36, Sidney Urknob dakika ya 42 na Mrisho Ngasa dakika ya 65.

Huu ni mchezo wa kwanza kati ya miwili ambayo Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera anataka timu icheze kwa ajili ya kusuka kikosi cha maangamizi Jumamosi uwanja wa Taifa dhidi ya Township Rollers.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com