Yanga yaipiku Simba kwa kumsajili Kakolanya kwa gharama hizi…


wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC wamefanikiwa kumsainisha kipa wa Prisons ya Mbeya na Taifa Stars, Benno Kakolanya mkataba wa miaka miwili.

Usajili huo ni pigo kwa Simba SC ambao pia walikuwa wanamtaka kipa huyo, lakini ‘Chelewa Chelewa, mwana si wao tena” – kwani wenye kisu kikali wamefanya yao.

Kakolanya amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu Prisons ya Mbeya.
“Nimesaini miaka miwili kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prsons,”amesema kakolanya ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Benno-Kakolanya-Kipa-Tanzanian-Prisons-goli-mbeya-city-bongosoka

Alipohojiwa pia na mtandao mwingine wa michezo wa boiplus , Kakolanya  alikiri kukamilisha ‘dili’ huku akiweka wazi ada ya kusaini kuwa ni Sh 35 milioni na mshahara Sh 1 milioni kwa mwezi.

Kakolanya alionyesha uwezo mkubwa msimu huu akicheza mechi 19 za ligi kuu na kufungwa mabao manane tu huku akiisaidia Prisons kumaliza katika nafasi ya nne mbele ya Mtibwa iliyomaliza ikiwa nafasi ya tano.
Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com