Yanga yaiua Mtibwa Sugar Morogoro , yavunja rekodi..


Vinara wa ligi kuu ya vodacom na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga SC wameendelea kufuta uteja uliokuwa umejengeka katika miaka ya hivi karibuni baada ya leo kufanya kile walichofanya dhidi ya Simba SC. Yanga SC ikiwa haijawahi kuifunga Mtibwa sugar katika miaka 5 ya hivi karibuni katika uwanja wa Jamhuri Morogoro, leo wamevunja mwiko huo na kufanikiwa kuwafunga Mtibwa sugar goli 2-0 ukiwa ni mwendelezo wa ushindi wake wa tano mfululizo katika ligi kuu ya vodacom. Katika mchezo wa leo ambao ulishuhudia timu hizo zikienda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana huku kukiwa na nafasi chache zilizo tengenzwa katika kipindi hicho cha kwanza.

Busungu-Yanga-Mtibwa-sugar-bongosoka

Yanga SC waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 53 kupitia kwa Malim Busungu akitumia uzembe a beki wa Mtibwa sugar ambaye alishindwa kuutoa mpira nnje na hatimaye Busungu akaunasa ule mpira katikati ya beki huyo na kipa wa Mtibwa Sugar Said Mohammed.
Kuingia kwa goli hilo kuliamsha kasi ya Mtibwa sugar kusaka goli la kusawazisha lakini jitihada zao ziligonga mwamba kufuatia uimara wa safu ya ulinzi wa yanga sc. Wakati mchezo ukielekea ukingoni Donald Ngoma aliifungia yanga sc goli la pili na kuihakikishia pointi zote tatu yanga sc katika mchezo huo. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Yanga kupata ushindi dhidi ya Mtibwa sugar katika uwanja wa Jamhuri ndani ya kipindi hiki cha miaka mitano.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com