Yanga yakamilisha usajili wa straika kutoka Gor Mahia


Klabu ya Yanga imefanikiwa kukamilisha usajili wa aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya ,  Yikpe Gislain Gnamien .

Mshambuliaji huyo tayari ameshamwaga wino wa kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka miwili huku akipewa jezi namba 9 .

Mshambuliaji huyu raia wa Ivory Coast anaiacha Gor Mahia baada ya klabu hiyo kuandamwa na matatizo ya kifedha huku akiwa na malimbikizo ya mshahara .

Gor Mahia walimsajili Yikpe kutoka SC Gagnoa mwezi July, mwaka 2019 kama mbadala wa Jacques Tuyisenge ambaye alijiunga na klabu ya \ Petro de Atletico ya Angola mwezi huohuo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com