Yanga yatoshana nguvu na Malindi


Katika Mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu visiwani Zanzibar . klabu ya Yanga iliweza kulazimishwa sare kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Malindi SC mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Deus Kaseke ndio alialitangulia kuifungia Yanga SC bao dakika ya 16 kabla ya Mohammed Ahmed Adam kuchomoa ushindi kwa yanga dakika ya 90.

Michezo mingine ya kujiandaa na Msimu mpya , Yanga ilitoa sare ya 1-1 na Kariobangi Sharks ya Kenya, ilishinda 2-0 dhidi ya Friends Rangers jana, 7-0 dhidi ya ATN, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 1-0 dhidi ya Mawenzi Market zote mjini Morogoro.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com