Yanga yatundikwa 2 – 0 na Mbao FC ….


Klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imeweza kuendeleza rekodi yake ya kuitungua Yanga kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2 – 0 kwenye mchezo wa mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba .

Magoli yote ya Mbao FC yalifungwa na  Habib Kiyombo   kunako dakika ya 53 na 68 ya mchezo huku mfungaji wa mabao hayo akifikisha jumla ya mabao 7 .

Baada ya kupoteza mchezo wa leo , Yanga inashuka hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 21 baada ya Singida United kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Njombe Mji na kufikisha pointi 23 .

Mbao FC inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya nane.

Hii inakua mechi ya kwanza kwa Yanga kupoteza baada  ya kucheza michezo 11 ya ligi bila kupoteza . Mbao FC inaendelea kuonyesha ungangari wa kukabiliana na vigogo wa ligi kuu baada ya kutoka suluhu na Azam FC na Simba huku ikiifunga Yanga kwenye mzunguko huu wa kwanza wa ligi kuu .

Ligi kuu inategemea kuendelea hapo kesho kwa mchezo mmoja ambapo Mbeya City itaikaribisha Kagera Sugar kabla ya kwenda mapumziko kwa ajili ya kombe la mapinduzi na michuano ya kimataifa .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com